Skip to main content
Tangazo la Mnada

TANGAZO LA MNADA WA MALI ZA SHIRIKA (KWA NJIA YA MAOMBI)

Shirika la Health & Insurance Management Services Organization (HIMSO) linawatangazia wananchi wote mnada wa mali chakavu za shirika (Pikipiki). Mnada huu utafanyika kwa njia ya kutuma maombi ya bei.

1. Orodha ya Pikipiki Zinazouzwa

Pikipiki zinauzwa kama zilivyo. Shirika halitahusika na gharama yoyote baada ya mauzo kukamilika.

Aina ya PikipikiNamba ya PikipikiMaelezo ya Matengenezo Yanayohitajika

 

HONDA

MC195 BJJ

Inahitaji matengenezo ya Knock Engine, Tyre, na side mirror

 

HONDA

MC968 BWG

Inahitaji matengenezo ya Engine, Tyre, Shockup, Side mirror

 

HONDA

MC612 CRS

Inahitaji matengenezo ya side mirror, Bulb, gear box, Tyre na Shock up

2. Masharti na Maelezo ya Kushiriki

  • Ukaguzi wa Pikipiki: Waombaji wanaruhusiwa kuja kuzikagua pikipiki kabla ya kutuma maombi, kuanzia tarehe 19/05/2026 hadi 26/05/2026.

  • Gharama za Maombi: Kila ombi litagharimu kiasi cha Tsh 10,000/= (Elfu kumi tu). Fedha hii hairudishwi.

  • Uwasilishaji wa Maombi: Waombaji wanatakiwa kuandika barua rasmi ya maombi kwenda kwa:

  • HEALTH & INSURANCE MANAGEMENT SERVICES ORGANIZATION (HIMSO) 01 Jacaranda, P.O. Box 2827, 53107 Mbeya, Tanzania 
  • Maudhui ya Barua: Barua lazima ionyeshe Namba ya usajili ya pikipiki inayotaka kununuliwa pamoja na Gharama/Bei ambayo mwombaji yuko tayari kununulia.

  • Njia ya Utumaji: Maombi yatumwe kwa njia ya barua pepe (Email): info@himso.or.tz 

3. Maelezo ya Malipo ya Maombi

Fedha za maombi zilipwe kupitia benki ya CRDB:

  • Jina la Akaunti: HIMSO 

  • Namba ya Akaunti: 0150290479807 

    Kumbuka kuambatanisha ushahidi wa malipo (Bank Slip/Screenshot) kwenye barua yako ya maombi.

4. Utaratibu kwa Washindi

  • Washindi watataarifiwa ili waweze kukamilisha malipo ya pikipiki walizoshinda.

  • Asilimia 50% ya malipo itatakiwa ilipwe papo hapo, na 50% inayobakia ilipwe ndani ya siku kumi na nne (14).

5. Mwisho wa Kupokea Maombi

Maombi yote yanatakiwa kuwa yamewasilishwa kabla ya tarehe 29/05/2026, saa 11.00 jioni. Maombi yatakayowasilishwa baada ya muda huo hayatozingatiwa.

 

Mawasiliano Zaidi

Kwa maswali au ufafanuzi zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia:

  • Barua Pepe: info@himso.or.tz 

  • Simu: 0761 555 552 

IMETOLEWA NA: Uongozi wa HIMSO, Makao Makuu, Mbeya.

Category: Announcements

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

HIMSO is a Tanzanian NGO established to complement the government’s efforts in providing comprehensive quality healthcare coverage as well as develop and implement innovative insurance solutions to address pressing risk management needs of the low-income households.

Recent News

Contact info